Saturday, 27 June 2015

NYOYO ZETU ZIPOLANDA

Upweke wa jinamizi

Halina hofu kwa maghani

Wangu moyo wakuandama

Tena kwako kwa mahaba.

Nyoyo zetu zipolanda

Vipi yasi tamua?



Majira za machweo

Subira ndo matokeo

Hisia za mgongomano

Nishajua mapenzi mirimo.

Nyoyo zetu zipolanda

Vipi yasi tamua?





Wangu mali rahani

Kwa haki si utani

Wangu roho pwaguzi

Kwa shairi ntarai.

Nyoyo zetu zipolanda

Vipi yasi tamua?





 © Robins 2014