Siku baki kenda
natua mpendwa
sitie shaka
sicheze mbali naja
Ishara na nne
siku kufika arubaine
zangu kawadia
japo nasinzia;
kwako naning'inia
sicheze mbali malkia
Mwendo ni wa kuvutia
hamna haraka,zawadia
japo moyo twajivunia
kwa umbali bara kanusia
sicheze mbali nakaribia
naja kwa mashua
punde ntatua
shada la maua ntapokea
bandarini kunipokea
sicheze mbali nakaribia
Sifi majini
nisizikwe vumbini
nife niwe hali jamani
siseme burhani
sicheze mbali
najivutia Unipe loniandalia
japo nasinzia
kuwaza na kuwazua
safari yote
hadi kutua
sicheze mbali
nakuamkia
© Robins 2014
No comments:
Post a Comment